• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Muundo wa Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Ujumbe Kutoka Kwa Mtendaji Mkuu
  • Kurugenzi na Vitengo
    • Kurugenzi ya Huduma na Uendeshaji
    • Kurugenzi ya Barabara za Mijini
    • Kurugenzi ya Barabara za Vijijini
    • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
    • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
    • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
    • Sehemu ya TEHAMA
    • Sehemu ya Mipango
    • Kitengo cha Sheria
    • Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu
    • Kitengo cha udhibiti Ubora na Utafiti
  • Miradi
    • Miradi yote
    • Miradi iliyo kamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ilio chini ya Ununuzi
    • Miradi ilio chini ya kubuni
  • Utawala
    • Bodi ya Wakurugenzi
    • Msimamizi Mkuu
    • Viongozi wa Idara
    • Waratibu wa Mikoa
    • Meneja wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Muongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Vifungu
    • Fomu za Maombi
  • Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video
    • Habari
    • Matukio
    • Maktaba ya Picha
  • Manunuzi
    • Taarifa ya Manunuzi
    • Zabuni za Wazi
    • Zabuni za juu
    • Tuzo za Zabuni
    • Kumbukumbu za Zabuni
  • Mitandao ya Barabara
    • Mitandao ya Barabara za Tarura
  • Mikoa
    • Waratibu wa Mikoa
    • Meneja wa Halmashauri

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS TAMISEMI MH. SULEIMANI JAFFO AWAAGIZA WATENDAJI WA TARURA KUFANYA KAZI KWA BIDII

Posted on: June 14th, 2018

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. Suleiman S. Jaffo, amehudhuria hafla ya uzinduzi wa magari 26 ya Wakala Wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ambayo yatakuwa yakitumika katika shughuli za usimamizi wa miradi ya barabara iliyo chini ya Wakala. Hafla hii ilifanyika siku ya Jumatano tarehe 13/06/2018 katika viwanja vya TARURA Makao Makuu kwenye jengo la PSPF Barabara ya kuelekea Chuo Kikuu cha Dodoma ambapo Mh. Jaffo alikuwa Mgeni rasmi.

Walioalikwa kuhudhuria hafla hii ni pamoja na Watumishi wa TARURA Makao Makuu, OR-TAMISEMI, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) Ofisi ya Mratibu wa TARURA Mkoa wa Dodoma,  Wawakilishi wa Benki ya NMB na Meneja wa TARURA  wa Jiji la Dodoma.

Katika hotuba aliyoitoa Mh. Suleimani Jaffo  hapa nanukuu, “Watumishi wa TARURA wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha TARURA inaendelea kuwa na jina zuri kwa Watanzania, kwa kuwa ukichafuka mwanzoni hata kama utajisafisha bado huwezi kuonekana safi”

Mh. Suleimani Jaffo aliendelea kuwaasa watumishi wote   kufanya  kazi kwa bidii na kwa kujituma   na wote wasiokuwa na maadili ya kazi, wenye roho mbaya, chuki na wasiokuwa na uzalendo kwa TARURA na Taifa hawatakiwi.

Aidha  Mh. Jaffo  alimshauri Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor H. Seff kuanzisha kitengo kipya cha usimamizi wa mikataba (Contract Management) ili kuhakikisha mikataba yote inayoingiwa na Wakala  inasimamiwa vizuri na kwa kufuata sheria na taratibu za manunuzi ya ya Umma.  Alisisitiza pia   Wakala uhakikishe kuwa  “Wakandarasi wanaoingia mikataba  na Wakala wanakidhi vigezo vya kiuhandisi ili kuepusha wakala usipate hasara ya kulipa gharama hapo baadae endapo Mkandarasi atashindwa kutekeleza yaliyomo kwenye mikataba.

Pia amewaagiza viongozi wa Wakala kuhakikisha magari yaliyonunuliwa yanatunzwa na kufanyiwa matengenezo kwa wakati ili yaweze kudumu kwa muda mrefu kwa kuwa yameigarimu Serikali fedha nyingi na pia akawaasa madereva wote wanao kabidhiwa magari kuhakikisha wanayatunza na kuyajali.

Vilevile   aliendelea kusisitiza umuhimu wa kuwa na taarifa sahihi  za  Mtandao wa Barabara ambao unakadiriwa kuwa na takribani zaidi ya kilomita 124,000, ambapo alipongeza wataalam wanaohusika na kusimamia mifumo ya  usimamizi wa taarifa za barabara (DROMAS) ili kuharakisha urasimishwaji wa Mtandao wa Barabara zilizopo chini ya Wakala.

Naye Mtendaji Mkuu wa  Wakala Mhandisi Victor H. Seff  kabla ya  kumkaribisha  Mgeni rasmi,  alitoa taarifa fupi ya upatikanaji wa magari hayo.  Alieleza kwa  Wakala unahitaji angalao magari 440 ili uweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Katika taarifa hiyo alieleza  kuwa wakala kwa sasa una magari 262 kati ya hayo 221 hali yake ni nzuri na yanatembea na magari 41 hali yake ni mbaya na yanatumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya matengenezo. Aliendelea kusema kuwa upatikanaji wa magari 26 utakuwa umesaidia kwa kiasi kikubwa kukabili changamoto hizo.

Vile vile alieleza kuwa ili kukabiliana na changamoto hizo za magari kwa mwaka wa fedha 2018/19 wakala umetenga kiasi cha shilingi  bilioni 2 kwa ajili ya ununuzi wa magari 20.

 

Matangazo

  • INVITATION FOR TENDERS -TARURA DEVELOPMENT ROAD WORKS PROJECTS IN TABORA REGION November 16, 2018
  • INVITATION FOR TENDERS (IFT) November 14, 2018
  • TANGAZO LA ZABUNI YA KUPATA WAKALA WA UKUSANYAJI WA MAPATO WA MAEGESHO YA MAGARI KATIKA HALMASHAURI ZA JIJI LA DAR ES SALAAM October 17, 2018
  • TANGAZO LA ZABUNI YA UNUNUZI WA MASHINE 1500 ZA KUKUSANYA MAPATO -POS(POINT OF SALE MASHINE) October 17, 2018
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Mawasiliano yarejeshwa kwa Wananchi wa Chinangali II na Mlebe

    January 03, 2019
  • TAARIFA KWA UMMA

    December 06, 2018
  • WAZIRI JAFFO ARIDHISHWA NA KAZI ZA TARURA

    July 25, 2018
  • UZINDUZI WA UPIMAJI KWA HIARI VVU/UKIMWI KWA WATUMISHI WA TARURA

    June 27, 2018
  • Angalia zote

Video

TARURA YATOA ELIMU KWA WANANCHI NANENANE SIMIYU 2018
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Tarura Barua pepe za Watumishi

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Ikulu
  • OR-TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Wakala wa Barabara

Waliotembelea duniani

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    TANZANIA RURAL AND URBAN ROADS AGENCY (TARURA),PSPF BUILDING 8TH FLR, DODOMA PLOT NO. 2 & 4 BLOCK G.

    Anuani ya Posta: P.O BOX 11042, DODOMA

    Simu ya mezani: 026-2963846

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: ceo@tarura.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Waliotembelea

StatCounter

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki @2017 TARURA. Haki zote zimehifadhiwa