• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Muundo wa Taasisi
    • Dira na Dhima
  • Miradi na Programu
    • Miradi iliyo kamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyochini ya Ununuzi
  • Utawala
    • Kurugenzi ya Huduma na Uendeshaji
    • Kurugenzi ya Barabara za Vijijini
    • Kurugenzi ya Barabara za Mijini
    • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
    • Kitengo cha Huduma za Sheria
    • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
    • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
    • Kitengo cha udhibiti Ubora na Utafiti
    • Sehemu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA)
    • Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu
    • Sehemu ya Mipango
    • Waratibu wa Mikoa
    • Mameneja wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Fomu Mbalimbali
    • Majarida
    • Vipeperushi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video
    • Habari
    • Matukio
    • Maktaba ya Picha
  • Manunuzi
    • Taarifa ya Manunuzi
    • Zabuni za Wazi
    • Tuzo za Zabuni
  • Mitandao ya Barabara
    • Mitandao ya Barabara za Tarura
  • Mikoa
    • Waratibu wa Mikoa
    • Mameneja wa Halmashauri

Waziri Jafo akabidhi Magari kwa TARURA

Posted on: November 14th, 2019

Na Bebi Kapenya

WAZIRI JAFO AKABIDHI MAGARI KWA TARURA YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 2.2 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo (MB), amekabidhi magari 22 yenye thamani ya Shilingi bilioni 2.2 kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), yaliyonunuliwa na Serikali kupitia Mfuko wa Barabara (RFB), ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali katika kukabiliana na changamoto ya vitendea kazi ambavyo imekuwa kikwazo kwa Wahandisi wa TARURA katika kufanya usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya barabara hasa maeneo ya vijijini.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi magari hayo iliyofanyika katika viwanja vya jengo la PSSSF ilipo Makao Makuu ya TARURA jijini Dodoma Novemba 13, 2019, Mhe. Jafo alisema kuwa, magari hayo yataenda kuongeza ufanisi katika kusimamia na kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara kwenye maeneo ambayo miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja inatekelezwa.

“Mwaka jana katika awamu ya kwanza nilikabidhi magari 26 na awamu hii ya pili ninakabidhi magari 22 jumla yatakuwa 48, imani yangu ni kwamba magari haya yatakwenda kusaidia kazi kubwa kufanyika kwa kutembelea maeneo yenye miradi ya wananchi na kutatua kero za wananchi”, amesema Mhe. Jafo.

Pia, Mhe. Waziri aliwataka madereva kuhakikisha kuwa wanayatunza magari hayo na kuhakikisha yanafanyiwa matengenezo ya mara kwa mara ili yaweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu, na aliwaasa viongozi wa TARURA kutolazimisha kutumia magari yaliyopitisha muda wa matengenezo kwani inapelekea magari mengi kuharibika katika kipindi kifupi.

Aidha, Mhe. Jafo aliipongeza TARURA kwa kazi nzuri wanayoifanya ya ujenzi na matengenezo ya barabara na pia kwa ujenzi wa ofisi ya Makao Makuu ya Wakala katika mji wa Serikali Mtumba.

“Nawapongeza TARURA kwa kazi nzuri mnayoifanya, kila ninapopita Wabunge wanasifu kazi yenu nzuri, japo rasilimali fedha ni ndogo lakini mnafanya kazi vizuri, pia nawapongeza kwa ujenzi wa jengo lenu la Ofisi ya Makao Makuu katika Mji wa Serikali Mtumba na nawaomba mhakikishe kazi inafanyika usiku na mchana ili jengo lenu liweze kukamilika kwa haraka na tunatarajia Mhe. Rais atakapokuja Dodoma ikimpendeza aweze kulizindua”, amesema Mhe. Waziri.

Katika hatua nyingine, Mhe. Waziri aliipongeza Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwasisitiza kuendelea kuangalia upya mgawanyo wa asilimia 30 unaopata TARURA kwani Wakala unahudumia mtandao wa kilomita 135,000 na fedha inayotolewa haitoshelezi katika kuunganisha vizuri mtandao wa barabara kwenye maeneo ya uzalishaji na  kuwawezesha wananchi katika maeneo hayo kuboresha shughuli zao za kiuchumi na kijamii.

“Angalieni vizuri kwa jicho la ukaribu, Wakala ni mpya na unafanya kazi nzuri na sasa unahudumia mtandao wa barabara zaidi ya kilomita 135,000, haiwezekani bado tukaendelea na mgawanyo wa asilimia 70 kwa asilimia 30 wakati huko ndiko wananchi wanapoishi, mgawanyo huu urekebishwe angalau hata iwe asilimia 40 kwa 60 ili kuweza kusaidia kazi zifanyike vizuri”, amesema Mhe. Waziri.

Naye, Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff alieleza kuwa, bado kuna upungufu wa magari 337 kwa nchi nzima ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi, kwani kuna Halmashauri nyingine Wataalamu wa TARURA wanatembelea maeneo ya miradi ya ujenzi kwa miguu na wengine wanapanda mabasi ambapo inapelekea wakati mwingine kushindwa kufika maeneo ya ndani zaidi ili kuweza kutatua changamoto za wananchi na hata wakati mwingine kutowasimamia Wakandarasi kwa ukaribu zaidi. Hivyo basi, ununuzi wa magari hayo ni suluhisho litakaloweza kusaidia kusimamia miradi ya Wakala vizuri kwa kadri inavyotakiwa.

Serikali imekuwa ikitenga fedha kila mwaka kwa ajili ya ununuzi wa magari tangu TARURA ilipoanzishwa mwaka 2017 ambapo awamu ya kwanza yalinunuliwa magari 26 na sasa awamu ya pili yamenunuliwa magari 22 na kufikia magari 48 yenye thamani ya jumla ya Shilingi Bilioni 4.3. Katika awamu ya tatu, Serikali imeendelea kutenga fedha za ununuzi wa magari kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ambapo magari 19 yameagizwa na TARURA kupitia ufadhili wa Bodi ya Mfuko wa Barabara.

MWISHO.

Matangazo

  • INVITATION FOR TENDERS - DODOMA REGION October 25, 2019
  • INVITATION FOR TENDERS - PWANI REGION October 22, 2019
  • INVITATION FOR TENDERS - DAR ES SALAAM September 20, 2019
  • TANGAZO LA ZABUNI YA WAKALA WA UTOZAJI WA ADA ZA MAEGESHO YA VYOMBO VYA USAFIRI KWENYE HIFADHI ZA BARABARA ZA MANISPAA YA IRINGA September 20, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Waziri Jafo akabidhi Magari kwa TARURA

    November 14, 2019
  • WATAALAMU WA TARURA WAJENGEWA UWEZO JUU YA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA BARABARA

    October 04, 2019
  • MFUMO WA MALIPO SERIKALINI-MUSE

    July 12, 2019
  • Mhe. JAFO AONGOZA WATUMISHI WA TARURA KUAGA MIILI YA WENZAO

    June 26, 2019
  • Angalia zote

Video

Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Tarura Barua pepe za Watumishi

Tovuti Muhimu

  • Wakala wa Barabara
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • OR-TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wizara ya Ujenzi uchukuzi na mawasiliano
  • Utumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Baraza la Mitihani
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi

Waliotembelea duniani

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    TANZANIA RURAL AND URBAN ROADS AGENCY (TARURA),PSPF BUILDING 8TH FLR, DODOMA PLOT NO. 2 & 4 BLOCK G.

    Anuani ya Posta: P.O BOX 11042, DODOMA

    Simu ya mezani: 026-2963846

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: ceo@tarura.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Waliotembelea

StatCounter

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki @2017 TARURA. Haki zote zimehifadhiwa