• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Muundo wa Taasisi
    • Dira na Dhima
  • Miradi na Programu
    • Miradi iliyo kamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyochini ya Ununuzi
    • Project and Program
    • RISE - DEC 2020
  • Utawala
    • Kurugenzi ya Huduma na Uendeshaji
    • Kurugenzi ya Barabara za Vijijini
    • Kurugenzi ya Barabara za Mijini
    • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
    • Kitengo cha Huduma za Sheria
    • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
    • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
    • Kitengo cha udhibiti Ubora na Utafiti
    • Sehemu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA)
    • Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu
    • Sehemu ya Mipango
    • Waratibu wa Mikoa
    • Mameneja wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Fomu Mbalimbali
    • Majarida
    • Vipeperushi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video
    • Habari
    • Matukio
    • Maktaba ya Picha
  • Manunuzi
    • Taarifa ya Manunuzi
    • Zabuni za Wazi
    • Tuzo za Zabuni
  • Mitandao ya Barabara
    • Mitandao ya Barabara za Tarura
  • Mikoa
    • Waratibu wa Mikoa
    • Mameneja wa Halmashauri

TARURA YAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU MKOANI NJOMBE

Posted on: December 3rd, 2020

TARURA YAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU MKOANI NJOMBE

Na. Erick Mwanakulya.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), unaendelea kutekeleza miradi mbalimbali katika Mkoa wa Njombe ili kuwezesha wananchi kusafiri na kusafirisha bidhaa na mazao kwa urahisi kwa kipindi chote cha mwaka.

Akielezea utekelezaji wa miradi mbalimbali, Mratibu wa TARURA Mkoa wa Njombe, Mhandisi Ibrahim Kibassa ameeleza kuwa ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha Lami zinazotokana na Ahadi za Mhe. Rais umekamilika kwa asilimia 100 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Halmashauri ya Mji wa Makambako na kwa upande wa Halmashauri ya Mji wa Makete barabara hizo zimekamilika kwa asilimia 80.

“TARURA Mkoa wa Njombe inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Wilaya zote 4 pamoja na Halmashauri zote, kwa sasa tupo katika ujenzi wa Daraja la Luhuji lenye urefu wa Mita 22 lililopo Njombe Mji ili kuunganisha   Kata ya Ramadhan pamoja na Kata ya Mabatini, daraja hili limegharimu Shilingi Milioni 514”, alisema Mhandisi Kibassa.

Aidha, ameeleza kuwa daraja hilo la Luhuji lilitakiwa kukamilika mwezi Novemba, 2020 lakini kutokana na changamoto za mvua Mkandarasi ambaye ni Pripam Company Ltd ameongezerwa Kipindi cha Mwezi mmoja ili aweze kukamilisha ujenzi wa daraja hilo.

Naye, Mwenyekiti wa Mtaa wa Ramadhan Bw. Festo Mwimba amesema kuwa, mtaa huo umekuwa na changamoto ya ukosefu wa daraja kwa muda mrefu na wamekuwa wakipata wakati mgumu kipindi cha masika hasa wanafunzi wa shule kuvuka kwenda upande wa pili hali iliyopelekea wengine kupoteza maisha na ameipongeza TARURA kwa kujenga daraja hilo la kudumu ili kutatua kero za wananchi.

Wakizungumza katika mahojiano maalum kwa nyakati tofauti Meneja wa TARURA katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Mhandisi John Kawogo alisema kuwa kabla ya TARURA kuanzishwa maeneo mengi yalikuwa hayawezi kupitika na wananchi wa Matamba, Kinyiko pamoja na Kikondo walishindwa kusafirisha mazao yao, ambapo kwa sasa barabara zote zinapitika kipindi chote na eneo linaloonekana kuwa korofi TARURA inafika kwa wakati ili kufanya matengenezo na kuhakikisha wananchi wanapita bila usumbufu.

“Kuna maeneo yalikuwa hayapitiki kabisa kama Kijiji cha Kipengele, eneo lile ulikuwa huwezi kupita ila kwa sasa barabara zinapitika kwa kipindi chote cha mwaka mzima”, alisema Mhandisi Kawogo.

Naye, Imaculata Msigwa Mkazi wa Mji wa Makambako, ameipongeza TARURA kwa kujenga barabara kwa kiwango cha lami na kwamba kwa sasa ni rahisi sana wananchi kufikisha mazao yao sokoni hasa katika Soko la Nyanya.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika Mkoa wa Njombe unaendelea kusimamia Mtandao wa Barabara zenye urefu wa Km 5208.58 katika Halmashauri zote 6 ili ziweze kupitika  kipindi chote cha mwaka kwa kutekeleza ujenzi wa mifereji, vivuko pamoja na maboresho ya miundombinu hiyo.

Matangazo

  • INVITATION FOR LOGO DESIGN COMPETITION November 12, 2020
  • SHINDANO LA KUANDAA NEMBO (LOGO) YA TARURA-KISWAHILI November 12, 2020
  • WALIOITWA KWENYE USAILI KADA YA UDEREVA TARURA MKOA WA TANGA November 06, 2020
  • KUITWA KWENYE USAILI-KIGOMA October 30, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • TARURA WAHIMIZWA KUONGEZA KASI YA UTENDAJI KAZI

    December 17, 2020
  • TARURA WILAYANI LIWALE YATEKELEZA MIRADI YA AHADI ZA VIONGOZI

    December 10, 2020
  • TARURA YAPONGEZWA UJENZI WA DARAJA LA KANKWALE MKOANI RUKWA

    December 08, 2020
  • BILLION 7.4 ZATUMIKA KUING’ARISHA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MPANDA

    December 07, 2020
  • Angalia zote

Video

Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Tarura Barua pepe za Watumishi

Tovuti Muhimu

  • Wakala wa Barabara
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • OR-TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wizara ya Ujenzi uchukuzi na mawasiliano
  • Utumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Baraza la Mitihani
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Instragram_tarura
  • twitter_tarura

Waliotembelea duniani

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    TANZANIA RURAL AND URBAN ROADS AGENCY (TARURA),TARURA HOUSE GOVERNMENT CITY -MTUMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 11042, DODOMA

    Simu ya mezani: 026-2963846

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: ceo@tarura.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Waliotembelea

StatCounter

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki @2017 TARURA. Haki zote zimehifadhiwa