• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Muundo wa Taasisi
    • Dira na Dhima
  • Miradi na Programu
    • Miradi iliyo kamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyochini ya Ununuzi
    • Project and Program
    • RISE - DEC 2020
  • Utawala
    • Kurugenzi ya Huduma na Uendeshaji
    • Kurugenzi ya Barabara za Vijijini
    • Kurugenzi ya Barabara za Mijini
    • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
    • Kitengo cha Huduma za Sheria
    • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
    • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
    • Kitengo cha udhibiti Ubora na Utafiti
    • Sehemu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA)
    • Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu
    • Sehemu ya Mipango
    • Waratibu wa Mikoa
    • Mameneja wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Fomu Mbalimbali
    • Majarida
    • Vipeperushi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video
    • Habari
    • Matukio
    • Maktaba ya Picha
  • Manunuzi
    • Taarifa ya Manunuzi
    • Zabuni za Wazi
    • Tuzo za Zabuni
  • Mitandao ya Barabara
    • Mitandao ya Barabara za Tarura
  • Mikoa
    • Waratibu wa Mikoa
    • Mameneja wa Halmashauri

MKANDARASI ATAKIWA KUMALIZA UJENZI WA BARABARA ZA MJI WA SERIKALI IFIKAPO JULAI 2021

Posted on: November 27th, 2020

MKANDARASI ATAKIWA KUMALIZA UJENZI WA BARABARA ZA MJI WA SERIKALI IFIKAPO JULAI 2021

 Na. Bebi Kapenya 

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor H. Seff amemuagiza Mkandarasi Kampuni ya China Heinan International Cooperation Co. Ltd (CHICO) anayetekeleza Mradi wa ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha Lami zenye urefu wa Km 51.2 katika Mji wa Serikali Mtumba kukamilisha kazi kwa muda na katika viwango vinavyotakiwa ifikapo tarehe 31 Julai 2021.

Mhandisi Seff ametoa agizo hilo wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa barabara hizo zinazoendelea kujengwa katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma na kubaini kuwa kuna ucheleweshaji wa muda uliowekwa kwa asilimia mbili (2%) kwani ujenzi umefikia asilimia 54 ambapo kwa mujibu wa ratiba ilitakiwa kufikia asilimia 56.

“Kimsingi suala la kuongezewa muda halipo kabisa kwenye huu ucheleweshaji wa asilimia 2, hakikisheni mnaongeza nguvu ya kufanya kazi na kuhakikisha mnamaliza kwa wakati kulingana na mkataba na ifahamike wazi kuwa kushindwa kukamilisha kwa wakati itapelkea kupewa adhabu kwa kukatwa kiasi cha fedha kama ilivyoainishwa kwenye mkataba”, alisema Mhandisi Seff.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa ujenzi wa barabara hizo unaogharimu Shilingi Bilioni 88.1 unahusisha ujenzi wa barabara za njia nne zenye urefu wa Km 11.2, ujenzi wa njia mbili zenye urefu wa Km 28.8, ujenzi wa kalavati, ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua, ujenzi wa barabara za waenda kwa miguu pamoja na taa za barabarani.

Aidha, amemtaka Mkandarasi huyo kuongeza kasi katika uzalishaji wa “U drains” zinazotumika kwa ajili ya mifereji na kwamba badala ya kutumia njia moja tu wanatakiwa kutumia njia zote mbili ili kuendana na muda.

Pia, Mkandarasi huyo ameagizwa kuangalia suala la usalama na jinsi ya kuongoza magari kwasababu njia hizo bado zinatumika kwenda kwenye maofisi mbalimbali ya Serikali yaliyopo Mtumba.

“Kimsingi hatua ambazo zimewekwa katika suala zima la usalama katika kuwaelekeza madereva hazitoshi kabisa hivyo, nawaelekeza muweke vibao vya kutosha na alama za kutosha ili kuwaelekeza madereva kufika kwenye ofisi mbalimbali za Serikali”, alisema Mtendaji Mkuu huyo.

Mradi wa ujenzi wa Barabara za Mji wa Serikali Mtumba unaosimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), unatekelezwa na Mkandarasi China Heinan International Cooperation Co. Ltd (CHICO) kwa muda wa miezi 18 ambapo unatarajia kukamilika ifikapo tarehe 31 Julai 2021.

Matangazo

  • INVITATION FOR LOGO DESIGN COMPETITION November 12, 2020
  • SHINDANO LA KUANDAA NEMBO (LOGO) YA TARURA-KISWAHILI November 12, 2020
  • WALIOITWA KWENYE USAILI KADA YA UDEREVA TARURA MKOA WA TANGA November 06, 2020
  • KUITWA KWENYE USAILI-KIGOMA October 30, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • TARURA WAHIMIZWA KUONGEZA KASI YA UTENDAJI KAZI

    December 17, 2020
  • TARURA WILAYANI LIWALE YATEKELEZA MIRADI YA AHADI ZA VIONGOZI

    December 10, 2020
  • TARURA YAPONGEZWA UJENZI WA DARAJA LA KANKWALE MKOANI RUKWA

    December 08, 2020
  • BILLION 7.4 ZATUMIKA KUING’ARISHA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MPANDA

    December 07, 2020
  • Angalia zote

Video

Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Tarura Barua pepe za Watumishi

Tovuti Muhimu

  • Wakala wa Barabara
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • OR-TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wizara ya Ujenzi uchukuzi na mawasiliano
  • Utumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Baraza la Mitihani
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Instragram_tarura
  • twitter_tarura

Waliotembelea duniani

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    TANZANIA RURAL AND URBAN ROADS AGENCY (TARURA),TARURA HOUSE GOVERNMENT CITY -MTUMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 11042, DODOMA

    Simu ya mezani: 026-2963846

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: ceo@tarura.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Waliotembelea

StatCounter

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki @2017 TARURA. Haki zote zimehifadhiwa