• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Muundo wa Taasisi
    • Dira na Dhima
  • Miradi na Programu
    • Miradi iliyo kamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyochini ya Ununuzi
    • Project and Program
    • RISE - FEB- 2021
  • Utawala
    • Kurugenzi ya Huduma na Uendeshaji
    • Kurugenzi ya Barabara za Vijijini
    • Kurugenzi ya Barabara za Mijini
    • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
    • Kitengo cha Huduma za Sheria
    • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
    • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
    • Kitengo cha udhibiti Ubora na Utafiti
    • Sehemu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA)
    • Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu
    • Sehemu ya Mipango
    • Waratibu wa Mikoa
    • Mameneja wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Fomu Mbalimbali
    • Majarida
    • Vipeperushi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video
    • Habari
    • Matukio
    • Maktaba ya Picha
  • Manunuzi
    • Taarifa ya Manunuzi
    • Zabuni za Wazi
    • Tuzo za Zabuni
  • Mitandao ya Barabara
    • Mitandao ya Barabara za Tarura
  • Mikoa
    • Waratibu wa Mikoa
    • Mameneja wa Halmashauri

DARAJA LA MWASONGE KUUNGANISHA MISUNGWI NA NYAMAGANA

Posted on: February 22nd, 2021

DARAJA LA MWASONGE KUUNGANISHA MISUNGWI NA NYAMAGANA

Na. Erick Mwanakulya, Mwanza.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), mkoani Mwanza umedhamiria kuunganisha Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana kupitia ujenzi wa Daraja la Mwasongwe lililopo Mto Nyashishi ili kuwezesha wananchi kufanya shughuli zao za usafiri na usafirishaji kwa urahisi.

Hayo yamesemwa na Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Mhandisi Alzabron Kayungi katika mahojiano maalum kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Daraja hilo lililopo katika Barabara ya Kaluluma–Mwasonge–Nyashishi yenye urefu wa Km 7 iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, na Barabara ya Buhongwa–Mwasongwe yenye urefu wa Km 4 katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana.

“Daraja hili la Mwasonge lililopo Mto Nyashishi lina urefu wa Meta 60 na limefikia asilimia 65 kukamilika na litagharimu shilingi Bilioni 1.78, Daraja hili linaunganisha Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi na litakamilika mwanzoni wa mwezi Mei mwaka 2021”, alisema Mhandisi Kayungi.

Mhandisi Kayungi ameongeza kuwa  kuwa Wakazi wa Kijiji cha Mwasongwe kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi wanategemea daraja hilo ili kupata mahitaji yao kama mahitaji kama shule, hospitali na huduma nyingine za kijamii, huku Wakazi wa Nyamagana wanategemea malighafi za ujenzi kama Mawe, Mchanga, Kokoto kutoka katika Kijiji cha Mwasongwe hivyo uwepo wa daraja hilo litasaidia wananchi kufanya shughuli zao za kila siku kwa urahisi.

Ndugu Msani Said Faida Mkazi wa Kigongo Ferry, ameipongeza Serikali kupitia TARURA kwa Ujenzi wa Daraja hilo kwani litawasaidia kufanikisha kupata huduma zao za kijamii kama shule, hospitali pamoja na huduma ya masoko katika Soko la Buhongwa.

Amesema kuwa daraja lililopo kwa sasa ni la miti ambalo pia ni hatarishi kwa usalama wao katika kusafirisha bidhaa, pia katika kipindi cha masika wanatumia mtumbwi kuvuka ambapo si salama hali inayopelekea kukwamisha shughuli zao na kusababisha kuzunguka umbali mrefu kwa kupitia usagara ili kuweza kuzifikia huduma mbalimbali.

“Naishukuru sana Serikali kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), kwa ujenzi wa Daraja hili la Mwasongwe na kutusaidia kufika Buhongwa kwa urahisi, tulikuwa tunateseka katika uvukaji kwa kutumia Daraja hili la Miti na kipindi cha masika tulikuwa tunatumia Mitumbwi kuvuka ambapo haikuwa salama kwetu”, alisema Bw. Msani Faida.

Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana Mhandisi Mohamed Muanda amesema kuwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana wapo katika ujenzi wa Daraja la Fumagila lenye urefu wa Meta 30, lililopo katika Mto Nyashishi Kata ya Kishiri linalounganisha Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana, Halmashauri ya Wilaya Misungwi pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Magu ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 95 na kugharimu shilingi Milioni 552 mpaka kukamilika kwake.

“Daraja hili la Fumagila lililopo katika Mto Nyashishi katika barabara ya Kishiri – Fumagila limefikia asilimia 95 na ni muhimu kwa wakazi wa maeneo haya kwani kipindi cha masika ilikuwa tabu kuvuka, pia wakazi wa Magu, Misungwi wanategemea kupata huduma katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana Kata ya Kishiri, daraja hili ni mkombozi kwa wakazi wa maeneo haya kwa kuwa wanategemeana sana”, alisema Mhandisi Muanda.

Aidha, mbali na ujenzi wa Daraja la Fumagila na Mwasongwe Mratibu wa TARURA Mkoa wa Mwanza Mhandisi Gaston Gasana amesema kuwa kwa kutumia malighafi za ujenzi kama mawe zilizopo kwa wingi mkoani Mwanza wameweza kujenga Barabara za Mawe maeneo ya milimani zenye urefu wa Km 11 kwa gharama nafuu.

TARURA Mkoa wa Mwanza inahudumia mtandao wa barabara wenye urefu wa Km 8,628 katika Halmashauri zote 8 ambazo ni Nyamagana, Buchosa, Sengerema, Ukerewe, Ilemela, Magu, Misungwi pamoja na Kwimba ambapo kazi za maboresho na ujenzi wa Miundombinu katika Halmashauri zote zinaendelea ili kuwawezesha wananchi kufanya shughuli zao za usafirishaji na usafiri kwa urahisi na kuhakikisha barabara na madaraja zinapitika katika kipindi chote cha mwaka.

Matangazo

  • INVITATION FOR LOGO DESIGN COMPETITION November 12, 2020
  • SHINDANO LA KUANDAA NEMBO (LOGO) YA TARURA-KISWAHILI November 12, 2020
  • WALIOITWA KWENYE USAILI KADA YA UDEREVA TARURA MKOA WA TANGA November 06, 2020
  • KUITWA KWENYE USAILI-KIGOMA October 30, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DARAJA LA MWASONGE KUUNGANISHA MISUNGWI NA NYAMAGANA

    February 22, 2021
  • TARURA INAVYOBORESHA MIUNDOMBINU MKOA WA RUVUMA

    February 18, 2021
  • TARURA INAVYOENDELEA KUTATUA KERO KWA WANANCHI MKOANI DODOMA

    February 03, 2021
  • TARURA WAHIMIZWA KUONGEZA KASI YA UTENDAJI KAZI

    December 17, 2020
  • Angalia zote

Video

Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Tarura Barua pepe za Watumishi

Tovuti Muhimu

  • Wakala wa Barabara
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • OR-TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wizara ya Ujenzi uchukuzi na mawasiliano
  • Utumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Baraza la Mitihani
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Instragram_tarura
  • twitter_tarura

Waliotembelea duniani

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    TANZANIA RURAL AND URBAN ROADS AGENCY (TARURA),TARURA HOUSE GOVERNMENT CITY -MTUMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 11042, DODOMA

    Simu ya mezani: 026-2963846

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: ceo@tarura.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Waliotembelea

StatCounter

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki @2017 TARURA. Haki zote zimehifadhiwa